Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bosi NMB alamba Tuzo Uingereza

Ruth Zaipuna Nmb Bosi NMB alamba Tuzo Uingereza

Thu, 14 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna ametunukiwa Tuzo ya heshima ya Uongozi bora wa biashara kwenye Bara la Afrika kutokana na uongozi wake bora kwa Taasisi hiyo kubwa ya fedha kuliko zotenchini Tanzania ambapo Tuzo hiyo imetolewa wakati wa kilele cha mkutano wa maendeleo ya Afrika na Tuzo za Uongozi wa Biashara za Afrika (ABLA) kwenye Ukumbi wa House of Lords katika Bungela Uingereza.

Ruth ametunukiwa tuzo hiyo maalum ya "African Business Leadership Commendation Award" ya mwaka 2022 na Jarida la African Leadership kwa juhudi zake za kuifanya NMB kuwa mbele katika ujenzi wa Taifa na kuchangia kikamilifu katika kuboresha maisha ya Watanzania.

Jarida hili linaloshapishwa na Taasisi ya African Leadership Organisation yenye makao yake makuu London Uingereza, linaheshimika kwa kuyatangaza mafanikio ya Afrika duniani ambapo Mwenyekiti wake Dr. Ken Giama amesema ushindi wa Ruth ulitokana na mchakato uliozingatia sifa stahiki ambao ulifanywa na Timu ya uteuzi ya bodi ya Wahariri wa Taasisi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live