Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bombardier 10 zaagizwa Ethiopia kuboresha usafiri wa anga

7776 Cq5dam.web .750.750 1.jpeg TZW

Fri, 11 May 2018 Chanzo: bongo5.com

Wakati Tanzania ikipiga hatua ya ununuzi wa ndege tatu aina ya Bombardier Q400 kutoka Canada, tayari nchi ya Ethiopia nayo imeagiza ndege nyingine  10 aina hiyo ili kuimarisha usafiri wa anga nchini humo.



Taarifa iliyotolewa na mtandao wa kampuni hiyo mnamo Aprili 27, 2018 imeonesha kuwa nchi hiyo nimeshaweka oda ya ndege 10 ambapo oda hiyo inakadiliwa kuwa na gharama ya kiasi cha dola milioni 332 zaidi ya tsh bilioni 736.

Shirika la ndege la Ethiopia ndio shirika la ndege la kwanza barani Afrika kuagiza kwa wingi ndege za Bombardier ambapo hadi sasa inamiliki ndege 22 za Bombardier Q400.

Shirika hilo pia linatumia ndege hizo za Bombadier Q400 kwenye nchi za Togo na Malawi hii ni baada ya kuingia ubia na mashirika ya Asky na Malawi Airline.

Soma taarifa hiyo zaidi – Ethiopian Airlines signs firm purchase agreement for 10 Q400 aircraft

Loading...
Chanzo: bongo5.com