Kampuni ya usafiri ya taksi za mtandaoni ya Bolt Tanzania imesema kuwa biashara imekuwa ikikua kwa kasi licha ya changamoto zilizopatikana mwaka 2022
"Bolt inafurahia hatua ilizopiga na kufanikisha mwaka wa 2022 licha ya changamoto zilizojitokeza. Biashara imeendelea kupata ukuaji mkubwa na Bolt inaendelea kuwa njia inayopendelewa zaidi ya usafiri katika maeneo ya mijini nchini Tanzania," Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Bolt, Kenneth Micah, alisema katika taarifa yake.
Bolt imetoa taarifa yake ya mwisho ya mwaka 2022 huku ikionesha utendaji kazi sambamba na huduma zake muhimu zote inazotoa.
Taarifa hiyo imeonesha pia safari ndefu zaidi ya jumla ya mteja nchini ilikuwa zaidi ya kilomita 7,000, wakati wastani wa umbali ulikuwa kilomita 7. Huku vituo vya mwisho vya safari vikiwa ni Mlimani City Mall iliyopo Jijini Dar es Salaam, Gran MeliĆ” ya Arusha, Rock City Mall ya Mwanza na the Royal Village Hotel iliyopo Dodoma.