Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bolt kusitisha huduma zake leo

BOLT USAFIRI Bolt kusitisha huduma zake leo

Wed, 17 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kampuni ya usafiri kwa njia ya mtandao inayojulikana kwa jina la Bolt Tanzania imetangaz aakusitisha huduma ya usafiri binafsi wa magari kufuatia kutofikia makubalianao na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu (LATRA)

Kupitia taarifa maalumu iliyotolewa na Bolt jana Agosti 16, 2022 imesema kuwa pande zote mbili zimekuwa kwenye mazungumzo na vikao vya muda mrefu vilivolenga kutatua changamoto za kiuendeshaji ambavyo wamedai zimechukua muda mrefu kufikia muafaka hivyo kusababisha kuwapo kwa uhaba wa huduma hiyo nchini.

Imeeleza zaidi kuwa licha ya changamoto hizo Bolt iliendelea kutoa huduma kwa wananchi ikiwa na mategemeo ya kupata suluhisho la kudumu litakalo nusuru mazingira ya kiutendaji kwao.

Kwa mantiki hiyo kuanzia leo Agosti 17, kampuni hiyo inatarajiwa kuchukua hatua nyingine ikiwemo kusitisha kabisa huduma ya usafiri kwa wateja wanaofanya malipo taslimu na kusalia kwa wateja wanaolipa kwa kadi.

Taarifa hiyo imeongeza kusema maamuzi hayo magumu yamefikiwa wakiwa hawana njia mbadala ya kutatua suala hilo hadi pale sheria za uendeshaji zitakapo badilishwa na wahusika waku ambao ni LATRA huku wakitumaini kuwa kutakuwepo na suluhisho litakalotoa ahueni kwa pande zote kuweza kunufaika ikiwa ni pamoja na madereva na abiria.

Kwa upande wa serikali ya Tanzania imetangaza kuwa ukomo wa viwango vya makato ya kamisheni ya nauli za taksi mtandao kwa madereva vitabakia kuwa asilimia 15 kama vilivyopangwa mwezi April mwaka huu.

Taarifa ya mamlaka ya udhibiti usafiri wa ardhini nchini Tanzania LATRA imesema baadhi ya kampuni za teksi mtandao zilizokuwa zikitoza kamisheni ya asilimia 20 hadi 31 hazikuridhika na kiwango elekezi cha asilimia 15.

LATRA imethibitisha nia ya kampuni ya Bolt kufunga huduma zake za taksi mtadao nchini humo kuanzia leo Agosti 17.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live