Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodi za tumbaku kuzifikisha kampuni za ununuzi mahakamani

Bodi Za Tumbaku Kuzifikisha Kampuni Za Ununuzi Mahakamani Bodi za tumbaku kuzifikisha kampuni za ununuzi mahakamani

Tue, 10 Oct 2023 Chanzo: Mwananchi

Bodi ya Tumbaku nchini (TTB) inatarajia kuzifikisha mahakamani kampuni nne za kizawa za ununuzi wa tumbaku ambazo hazijamalizia kuwalipa wakulima kiasi cha Sh4.5 bilioni tangu.

Mkurugenzi Mkuu wa bodi hiyo Stan Mnozya ameyasema hayo leo Jumanne Oktoba 10, 2023; huku akibainisha kuwa muda wowote wiki hii, kampuni hizo zitafikishwa mahakamani iwapo zitakuwa hazijawalipa wakulima hao kesho Jumatano.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, TTB imekuwa katika mazungumzo na kampuni hizo bila mafanikio yeyote na kwamba sasa wanataka kuchukua hatua za kisheria dhidi yao.

"Hatukuwa na lengo hilo lakini baada ya vikao vya mara kwa mara na kuhimizana kulipa bila mafanikio, sasa tuliwapa siku saba na zinamalizika kesho Jumatano na baada ya hapo wasilaumu," amesema.

Mnozya amebainisha kuwa kuzifikisha kampuni hizo mahakamani, pia ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, alilolitoa mjini Urambo mwaka jana, baada ya kusikia kilio cha wakulima kutolipwa na kampuni za wazawa na hivyo kuagiza kampuni zitakazoshindwa kuwalipa wakulima zichukuliwe hatua za kisheria.

Chanzo: Mwananchi