Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodi yawafunza wakulima mikoa mipya ya korosho

376722c73de0f30e4802f2a200285c6b Bodi yawafunza wakulima mikoa mipya ya korosho

Thu, 25 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

BODI ya Korosho Tanzania (CBT), inatoa elimu kwa wakulima wa korosho katika mikoa mipya inayolima zao hilo ili kuwezesha kuanza ubanguaji wa zao hilo na kuepuka uuzaji wa korosho ghafi.

Kaimu Meneja Mipango ya Kilimo wa CBT, Juma Yusuph, alibainisha hayo hivi karibuni katika mafunzo ya ubanguaji wa korosho yaliyoandaliwa na bodi hiyo na kutekelezwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (Tari) Naliendele.

Kwa mujibu wa Yusuph, hadi sasa nchi inabangua asilimia 10 ya korosho zinazozalishwa nchini.

Alisema korosho ikibanguliwa inapata soko haraka ndani na nje ya nchi, lakini korosho ghafi zimekuwa zikichelewa kuuzwa kutokana na nchi mbili pekee za India na Viettenam kuwa ndizo wateja wakubwa.

"Taasisi hii imejikita kutoa elimu kwa wakulima wa korosho kwa mikoa mipya ili waanze kubangua korosho zao na kuondokana na uuzaji wa korosho ghafi nchini,” alisema.

“Tumieni haya mafunzo kama mwanzo wa mabadiliko ya jiitihada tunazowekeza katika kilimo cha korosho kutoka maeneo tunayoishi," alisema Yusuph.

Alisema wanafanya juhudi kuhakikisha kunakuwa na soko la uhakika, ingawa bado kiasi kinachobanguliwa ni kidogo ikilinganishwa na kinasafirishwa kwenda nje ya nchi.

"Ukibangua korosho unaweza kula, lakini usipobangua korosho huwezi kula; hapa nchini tunabangua chini ya asilimia 10 ndio maana tunatoa mafunzo na kuwapa mbinu za kuwawezesha nyie kufanya ubanguaji kwa vikundi kundi ili kuongeza pato la mkulima na kujenga soko endelevu litalowezesha kulisha korosho hizo kwa nchi jirani," alisema Yusuph.

Mtafiti wa Mbegu Bora za Korosho kutoka Tari- Naliendele, Dadili Majune, alisema ufundishwaji huo una tija kwa wakulima wa mikoa mipya inayolima korosho nchini, hivyo yasiishie kwa wakulima hao pekee, bali nao wawafundishe wakulima wenzao.

Mkulima Selemani Mohamed kutoka Dodoma, alisema elimu kuhusu zao la korosho inawasaidia kufahamu mfumo mzima wa uzalishaji zao hilo hivyo, naye atatoa elimu hiyo kwa wenzake ili wajue umuhimu kilimo cha korosho.

Chanzo: habarileo.co.tz