Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodi ya utalii kuanzisha ofisi Terminal III Dar

Mon, 10 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji mstaafu, Thomas Mihayo amesema bodi hiyo itakuwa na ofisi maalumu katika jengo jipya la kupokelea wageni (Terminal III) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.

Jaji Mihayo ameyasema hayo leo Jumatatu Juni 10 jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia jinsi bodi hiyo ilivyojipanga kutangaza utalii kwa wageni wanaowasili nchini, pia kutangaza utalii kwenye nchi wanazotoka.

“TTB tutapata ofisi ya kudumu katika jengo jipya la Terminal III na jukumu letu litakuwa ni kuwasaidia watalii wanapofika hapa nchini, kuwaeleza vivutio tulivyonavyo pamoja na kuwaunganisha na wadau wengine muhimu,” amesema Mihayo.

Mwenyekiti huyo amesema mbali na kuwa na ofisi, wataweka pia matangazo mbalimbali ya vivutio vya utalii kwenye uwanja huo ili kuvitangaza kwa wageni wanaoingia nchini kwa shughuli mbalimbali.

Kuhusu tuhuma za baadhi ya wabunge kwamba bodi hiyo imeshindwa kutangaza vivutio vya utalii kwenye mataifa mengine, Mihayo amesema siyo kweli kwa sababu wanajitahidi kutangaza licha ya kwamba bajeti inakuwa ndogo.

Amesema kupitia kwa mabalozi hao, wameanza kuona matokeo ya kuja kwa watalii wengi siku za hivi karibuni wakiwemo watalii 1000 kutoka Israel na watalii 345 kutoka China

Pia Soma

 

Chanzo: mwananchi.co.tz