Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodi ya pamba yapata mwarobaini kudhibiti wadudu

Pamba Bodi (600 X 353) Bodi ya pamba yapata mwarobaini kudhibiti wadudu

Mon, 7 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Balozi wa Pamba nchini Aggery Mwanri amesema kuwa Bodi ya Pamba imejipanga kikamilifu kukabiliana na wadudu washambuliao zao hilo, kwa kupeleka dawa za kutosha kwa wakulima na kuwafundisha jinsi ya kunyunyuzia.

Mwanri ametoa kauli hiyo leo, wakati wa zoezi lake la kuelimisha wananchi wa mkoa wa Simiyu ambao ni wakulima jinsi ya kunyunyuzia sumu hizo linaloendelea katika wilaya mbalimbali mkoani humo.

Amesema kuwa Uwezo, nguvu na nia ya kupambana na wadudu hao kwa bodi ya pamba upo, kwani wakulima wengi tayari wamesamaziwa dawa za kutosha ikiwemo na kupewa elimu ya jinsi ya kuzitumia.

Amesema kuwa kila mkulima atapewa elimu na atapata dawa kulingana na shamba alilolima, kwani dawa zipo za kutosha na wamejipanga katika msimu huu wa pamba kuhakikisha wadudu hao wanaangamizwa.

“ Kama serikali kupitia Bodi ya pamba, tumejipanga kwa nguvu zote kupambana na wadudu hawa, uwezo tunao, nguvu tunazo, na nia tunayo, tumejipanga kuhakikisha tunawaangamiza katika msimu wa mwaka huu” amesema Mwanri.

Balozi amewataka wakulima wote wanaopewa sumu hizo, kuhakikisha wanazitumia kwa kazi iliyokusudiwa huku akiwatahazarisha wale wote wenye nia ya kuchukua sumu na kwenda kuziuza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live