Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodi ya nafaka kuingia mikataba na wakulima baada ya kupata soko nje ya nchi

NAFAKAAAA Bodi ya nafaka kuingia mikataba na wakulima baada ya kupata soko nje ya nchi

Wed, 3 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bodi ya nafaka na mazao Mchanganyiko (CPB) imesema itaingia mikataba na wakulima wa mazao Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kufuatia kuwepo kwa mtandao wa masoko ya uhakika nje ya nchi.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi Mkuu bodi ya nafaka (CPB) Dkt. Anselm Moshi wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya 29 ya Sikukuu ya Wakulima (nane nane) yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.

Aidha, Dkt Moshi alisema kuwa wamekuwa na utaratibu wa kukusanya mazao ya wakulima kuyachakata na kuyaongezea thamani kupitia uwekezaki wa viwanda nane vya kuchakata mazao.

Akielezea zaidi Mkurugenzi huyo amesema kuwa njia ya pili ni mkulima kutumia mtandao mpana wa bodi ya nafaka Tanzania ambao upo ndani na nje ya nchi ambao upo, Congo, Comoro, Kenya, Uganda, Rwanda, Zimbabwe.

"Kwa hiyo tumeanza kujenga mtandao mkubwa wa kuuza mazao ya wakulima na tunaendelea kujenga huo uwezo wa kimtandao ili wakulima wa Tanzania wa alisema mazao ili bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko iweze kununua na kuhifadhi kwenye miundo mbinu yake" amesema Mkurugenzi huyo.

Hata hivyo Dkt.Moshi amesema wanataka wakulima wafahamu kuwa bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko ina bidhaa bora ambazo zimeandaliwa kwa umakini mkubwa Kwa kutumia watalaam wa bodi hiyo.

John Mwakinywa ni mkulima wa zao la Alizeti katika wilaya ya Mbeya Vijijini amesema kuwa uwepo wa bodi hiyo utakuwa msaada mkubwa Kwa wakulima.

"Tunaamini kuwa sisi tutapata Neema sasa na tutaweza kulima mazao yetu sasa kwa tija hii bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko ni Neema kwetu sasa tujikite kuzalisha kwa ubora" Amesema mkulima huyo.

Mkulima mwingine Peter Juma amesema kwamba kilimo kinatakiwa kiwe mkombozi kwa mkulima hivyo uwepo wa bodi hii utaweza kuwainua wakulima waliokata tamaa ya kilimo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live