Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodi ya mkonge yasaini makubaliano uwekezaji bil 14/-

7a4bc4b6076d81cec49e9ed87372ea0e Bodi ya mkonge yasaini makubaliano uwekezaji bil 14/-

Sat, 9 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

BODI ya Mkonge Tanzania (TSB) imesaini makubaliano na kampuni ya Grosso Sisal ya nchini Uholanzi iili iwekeze Dola za Marekani milioni sita (takribani shilingi bilioni 14 za Tanzania) kwa miaka mitatu kwenye zao la mkonge.

Uwekezaji huo utafanyika katika maeneo ya ununuzi wa mashine za kuchakata zao hilo na kuongeza mnyororo wa thamani wa zao hilo.

Akizungumza baada ya kusaini makubaliano hayo Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo Nuradin Osman alisema, lengo la kwanza la uwekezaji huo ni kuwasaidia wakulima wadogo kuweza kuongeza uzalishaji na kuunga mkono jitihada za Serikali kutimiza malengo yake kwenye zao hilo.

Makubaliano ya TSB na mwekezaji huyo yalisainiwa mwishoni mwa wiki kwenye ofisi za bodi hiyo jijini Tanga.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mkonge Tanzania, Marium Nkumbi alisema uwekezaji huo utasaidia wakulima kuchakata mkonge wao kwa urahisi kwani wataweza kuwa na mashine zenye uwezo.

Alisema kuwa licha ya kufanya jitihada kubwa kwenye uzalishaji lakini hapa nchini matumizi ya mkonge ni asilimia 2%pekee hivyo mwekezaji huyo anakuja kusaidia kuongeza thamani ya zao.

"Zao hili Lina vitu vingi ndani yake ikiwemo kutengeneza chakula cha mifugo, kuzalisha umeme hivyo kulingana na uwekezaji wake hapa nchini utasaidia ulimaji mkonge hapa nchini"alisema Nkumbi.

Kaimu Mkurugenzi wa bodi hiyo, Saad Kambona alisema lengo la Serikali linawataka mpaka ifikapo 2025 wawe wameongeza uzalishaji hadi kufikia tani 120,000 kwa mwaka kutoka uzalishaji wa tani 36,000 za sasa.

Chanzo: habarileo.co.tz