Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodi ya mazao yafungua fursa kwa wakulima

Manunuzi Bido Bodi ya mazao yafungua fursa kwa wakulima

Tue, 2 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakulima mikoa ya Nyanda za Juu Kusini wanatarajia kuanza kunufaika na mikataba ya manunuzi ya mazao kupitia Bodi ya Mazao ya Nafaka Mchanganyiko (CPB) ambayo yatachakatwa kuongezwa thamani na kuuzwa katika masomo ya nchi za Afrika Mashariki.

Mkurugenzi Mkuu wa bodi hiyo, Dk Anselm Moshi amesema hayo leo Jumanne Agosti 2, 2022 wakati akizungumza na Mwananchi kwenye banda la maonyesho ya 29 ya sikukuu ya wakulima maarufu nanenane ambayo Kitaifa yanafanyika katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Dk Moshi amesema kuwa ushiriki wao katika maonyesho ya nanenane Kitaifa ni kuwahakikishia  wakulima kuwepo kwa mtandao mkubwa wa masoko  kupitia bodi hiyo  kutokana na kuwepo kwa  uwekezaji mkubwa wa viwanda nane  vya kuchakata mazao na kuuza nje ya nchi.

''Tayari tuna mtandao mkubwa wa bodi ya nafaka katika nchi zote za Afrika mashariki hususan Comorro, Zambia, Kenya, Congo, Zimbabwe, Ulaya na nchi nyingine kwa ajili ya kuuza mazao ya wakulima wa Tanzania ''amesema.

Amesema lengo ni kuona namna gani wakulima na wadau wa kilimo wanatambua majukumu  CPB ikiwa ni pamoja na uwepo wa  huduma ya kupima kusafirisha na kuhifadhia ubora wa  mazao katika Mikoa ya Songwe, Iringa, Mwanza, Arusha, Dodoma, Ruvuma na mingineyo.

Ametaja miongoni mwa mazao ambayo yamekusanya kwa wakulima na kuchakatwa kuwa ni unga wa dona, sembe, mchele, mafuta ya kula ya alizeti, korosho kwa ujazo tofauti

Advertisement Mkulima wa  zao la alizeti kutoka banda la  maonyesho Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya, Daniel Naftari amesema uwepo wa maonyesho ya nanenane ni fursa pekee kwao kubaini uwepo wa masoko makubwa ya bidhaa na hivyo ni wakati wa kuunga mkono.

''Uwepo wa bodi ya mazao mchanganyiko wa kuingia mkataba na wakulima ni tija kubwa kwetu kuuza mazao hivyo na kuomba  kuwafikia maeneo ya vijijini kutoa elimu ili kutumia soko hilo kuuza mazao na kufanya biashara ya pamoja .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live