Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodi ya chai yazinduliwa Kilolo

Chai Melt Bodi ya chai yazinduliwa Kilolo

Wed, 11 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bodi ya Chai Tanzania (TBT), imezindua Bodi ya Kampuni ya Chai Kilolo itakayosimamia uendelezaji wa zao la chai katika Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuongeza mchango wa zao la chai katika Pato la Taifa.

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Chai Tanzania, Bi. Mary Kipeja amesema bodi hiyo itasaidia kuongeza ufanisi katika kusimamia zao la chai wilayani humo.

Kilolo ina mashamba makubwa ya chai yaliyokuwa yametelekezwa kwa zaidi ya miaka 30. Mashamba hayo yaliwekwa chini ya Bodi ya Chai ili kuhakikisha yanaanza uzalishaji.

“Leo sekta ya chai imeandika historia mpya kutokana na uzinduzi wa bodi ambayo inaenda kuleta mabadiliko katika sekta ya chai nchini, na niwahakikishie kuwa sekta inaenda kubadilika na kuwa kati ya sekta kubwa zenye tija kwa pato la taifa,” amesema Mary Kipeja.

Mbunge wa Jimbo la Kilolo Justine Nyamoga (CCM) alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Lain Kamendu atakuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi. -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live