Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodi ya Nafaka: Vita Ukraine, Russia chanzo uhaba wa chakula

Nafaka  NAFAKA Bodi ya Nafaka: Vita Ukraine, Russia chanzo uhaba wa chakula

Mon, 13 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB), Salum Awadh, amesema kupanda kwa chakula kunatokana na changamoto mbalimbali ikiwemo upatikanaji hafifu wa mbolea unaochangiwa na Vita ya Ukraine na Urusi.

Ametoa kauli hiyo Jijini Dar es Salaam katika mkutano wa Wadau wa Bodi hiyo ambapo mbali na jitihada hizo amesema kwa sasa Bodi inapanga kununua mazao kwa wingi kutoka kwa Wakulima na kuweka ziada ya chakula ambapo amesema Bodi hiyo inaweza kununua mazao yenye thamani ya Bilioni 50 huku ikitarajia kuongeza kiasi hicho cha fedha na kufikia Bilioni 100.

“Sisi tuna uwezo wa kununua mazao mpaka Bilioni 50 lakini bajeti yetu ya mwaka huu wa fedha unaoanza fedha tumeongeza bajeti mara mbili mpaka Bilioni 100”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live