Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodi ya Mkonge yajidhatiti kuongeza uzalishaji kufikia tani 120,000

Bodi Ya Mkonge Yajidhatiti Kuongeza Uzalishaji Kufikia Tani 120,000 Bodi ya Mkonge yajidhatiti kuongeza uzalishaji kufikia tani 120,000

Thu, 17 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bodi ya Mkonge Tanzania imesema ili kutimiza adhma ya Serikali na Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM itahakikisha inafikia lengo la uzalishaji wa mkonge unaongezeka hadi kufikia tani 120,000 kwa Mwaka, ifikapo Mwaka 2025/2026.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Katani Tanzania (TSB) Saddy Kambona katika mkutano na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO jijini Dodoma Agosti 16,2023.

Kambona amesema Zao la Mkonge likaingizwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2020-2025 ambamo limewekwa lengo la kuongeza uzalishaji kutoka tani 36,000 zilizokuwa zinazalishwa kwa Mwaka 2020 hadi kufikia tani 80,000 kwa Mwaka, ifikapo Mwaka 2025.

Hatua za Serikali kuliingiza zao la mkonge kwenye orodha ya mazao ya kimkakati ilitokana na ukweli kwamba mahitaji na soko la mkonge limezidi kuimarika duniani.

''Hatua za Serikali kuliingiza zao la mkonge kwenye orodha ya mazao ya kimkakati ilitokana na ukweli kwamba mahitaji na soko la mkonge limezidi kuimarika duniani''amesema Kambona

Pia ni kutokana na kugundulika kwa matumizi mapya ya Mkonge na uzalishaji wa bidhaa mpya zitokanazo na mkonge kama vile vifaa vya ujenzi(gypsum boards, Matofali,mbao, mabati, vigae), Sukari ya Mkonge, Pombe ya Mkonge, Karatasi maalum, Bio Gas, mbolea, Chakula cha mifugo , urembo, mabodi ya magari n.k.

Kambona amesema Mnamo mwaka 2019, uzalishaji wa Singa ulikuwa tani 36,324 na uzalishaji wa bidhaa ulikuwa 6,237.08 huku mwaka 2023, uzalishaji wa Singa ukiwa tani 34,630.54 na uzalishaji wa bidhaa ukiwa 401.53.

Fursa ya kilimo cha Mkonge ni nzuri kwa sababu ya bei na mahitaji yake, kuna fursa ya biashara ya kununua na kuuza mkonge na bidhaa za mkonge na utoaji huduma ya uchakati na utengenezaji wa chakula cha mkonge kibiashara ikiwemo chakula cha ng'ombe.

"Ni lazima kuendelea kuhamasisha wawekezaji mbalimbali kuwekeza katika viwanda vya kuongeza thamani katika mnyororo wa thamani wa zao la Mkonge ili kuongeza matumizi ya Mkonge nchini na hivyo kuchagiza kukua kwa kilimo cha mkonge.- Amesema Kambona

"Pia ni jukumu letu kulinda viwanda vichache vilivyopo kwani kwa sasa takriban asilimia 70% ya mkonge unauzwa nje kama malighafi/fiber (kabla ya kuongezwa thamani) kwenye nchi takriban 26." - Kambona

Hata hivyo amehitimisha kwa kusema Katani ya Tanzania ina ubora zaidi wa kutengenezwa sukari kuliko aina ya katani inayozalishwa Mexico.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live