Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodi ya Kahawa yajipanga kuongeza usalishaji Tanganyika

Bodi Ya Kahawa Yajipanga Kuongeza Usalishaji Tanganyika Bodi ya Kahawa yajipanga kuongeza usalishaji Tanganyika

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi Onesmo Buswelu amewataka wataalam wa kilimo kuhakikisha miche yote waliopewa wakulima wa zao la kahawa inapandwa na kulindwa ili kuongeza kasi ya wakulima kuingia katika kilimo cha zao hilo.

Buswelu ameyasema hayo katika zoezi la ugawaji wa miche zaidi ya laki tano ya zao la kahawa lililofanyika katika kijiji cha Mwese huku akiwahakikishia soko la uhakika wakulima wa zao hilo.

Taarifa iliyosomwa mbele ya mkuu wa wilaya hiyo inasema moja ya changamoto katika kilimo cha kahawa ni kulimwa na wazee kutokana na vijana kudaiwa kukimbia kilimo hicho huku Afisa Maendeleo wa zao hilo Kanda ya Magharibi amesema Bodi ya kahawa Tanzania imeweka mpango wa kuongeza uzalishaji wa zao la kahawa kitaifa.

Kwa upande wao wakulima waliopatiwa miche hio wameeleza mafanikio waliopata kutokana na kilimo cha kahawa.

Aidha wakulima wametakiwa kupokea ushauri na maelekezo ya watalaam ili kupata tija na ufanisi katika zao la kahawa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live