Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodi ya Kahawa yajipanga kufanya maboresho

KAHAWA Bodi ya Kahawa yajipanga kufanya maboresho

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakulima wa zao la kahawa katika kijiji cha Mwese halmashauri ya Tanganyika mkoani Katavi wamewaomba maafisa ugani kuwatembelea mara kwa mara katika mashamba yao ili kuwapa elimu ambayo itawasaidia kuongeza uzalishaji na kuwafanya wajikwamue kiuchumi .

Mbali na changamoto ya kutotembelewa na wataalamu wa kilimo pia wakulima hao wameiomba serikali kusogeza huduma ya pembejeo karibu na maeneo yao ya uzalishaji ili kuepuka gharama ya kufuata pembejeo njee ya zao la kahawa njee ya mkoa wa Katavi.

Afisa Mazao Halmashauri ya Tanganyika Sephania Waya amesema kwasasa muitikio wa wananchi kulima zao hilo ni mkubwa ikilinganishwa na hapo awali huku Afisa Maendeleo wa zao la Kahawa Kanda ya Magharibi Jasson Michael akidai matarajio yao ni kuongeza uzalishaji wa zao la kahawa kutoka tani 82 elfu hadi kufikia tani laki 3 kitaifa.

Aidha Michael amewataka wakulima na wawekezaji kutumia fursa iliyopo katika halmashauri ya Tanganyika kulima zao la kahawa kutokana na zao hilo kustawi maeneo mengi ya halmashauri hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live