Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bodaboda wachekelea Uber kusitisha huduma

Boda Boda 1 Bodaboda wachekelea Uber kusitisha huduma

Sun, 17 Apr 2022 Chanzo: eatv.tv

Ikiwa ni zimepita siku chache tangu Uber iwajulishe wateja wake kwamba imesitisha kutoa huduma zake za usafiri ambazo ni Uber X, Uber XL na Uber X Saver, raia wanaoendesha pikipiki kusafirisha abiria maarufu kama bodaboda Jijini Dar es Salaam wamesema hatua hii kwao ni sawa na "kufa kufaana"

Wakizungumza wafanyabiashara hao wamesema kuwa kwao taarifa hii imeleta neema kwao kwakuwa uwepo wa Uber uliifanya biashara kuwa ngumu sambamba na kuwanyonya wale waliokuwa wakitumia mfumo wa uber.

"Hawa jamaa walikuwa wanatunyonya mno, wao ni kana madalali kati yetu na mteja. Sisi tunakuwa hatupati faida, tunawafanyia wao. Kwahiyo kusema wanasitisha huduma sisi kwetu ni sawa kabisa kwasababu wanatunyonya mno. Wafunge tu hata wasirudi kwasababu wanatuharibia kazi na tunakuwa tunawafanyia wao" - Kelvin Joseph, dereva bajaji.

Aidha, mmoja wa waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda amesema kuwa kusitishwa kwa huduma ya Uber kutawafanya wapate kipato kulingana na bei halisi.

"Tunashukuru uber wamefunga huduma, walikuwa wametuharibia kazi kabisa. Mteja anagika hapa anasema mimi naenda Makongo lakini anataja bei za uber ambazo zinatuumiza kwahiyo unakuwa haupati faida, tunaomba waendelee kufunga sisi tufanye kazi" - Joseph Evans, bodaboda Dar es Salaam. 

Victoria Merikiadi, mtumiaji wa huduma ya Uber na mkazi wa Jiji la Dar es salaam anasema kwamba kusitishwa kwa huduma hii kunawaumiza watu waliokuwa wakitumia Uber hasa wa kipato kidogo wasio na magari.

"Sisi watu ambao hatuna magari ndio tunaenda kuteseka kitokana na uber kusitisha huduma, uber wamekuwa wakitusaidia sana kufika tunapokwenda kwa haraka na hata bei yao ni nzuri. Ninaiomba LATRA wakae na serikali kuona namna ya kupunguza gharama kwasababu uber ni mwanzo tu, wengine pia kama Bolt watajitoa na wao" - Victoria Merikiadi, mtumiaji wa Uber.

Chanzo: eatv.tv