Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

BoT yatoa tahadhari uwepo wa dola bandia

Dola Dola Juu Juu BoT yatoa tahadhari uwepo wa dola bandia

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imeagiza benki na maduka ya kubadili fedha za kigeni wachukue tahadhari kuepuka fedha feki za nchi za nje zikiwamo Dola za Marekani.

Taarifa ya Kurugenzi ya Usimamizi wa Sekta ya Fedha, BoT imetaja tahadhari hizo kuwa ni pamoja na kuimarisha mifumo ya kuzitambua noti feki za nje ya nchi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, BoT ilipata taarifa kuhusu kukamatwa kwa kiasi kikubwa cha noti feki za Dola za Marekani katika nchi za nje zilizokuwa zikiletwa barani Afrika.

“Pia benki zote na maduka ya kubadili fedha za kigeni wanashauriwa waendelee kuelimisha wateja kuhusu madhara ya kuwatumia watu wasiohusika katika biashara ya fedha za kigeni wakiwamo wanaoweza kuwa watengenezaji wa noti feki,” ilieleza taarifa hiyo.

Chama cha Benki Tanzania (TBA) kimetoa mwito kwa wananchi waepuke tamaa ya kumiliki dola bandia za Marekani.

Mwenyekiti wa TBA ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema hayo alipozungumza na HabariLEO jana.

Nsekela alisema tahadhari kwanza ni kwa wananchi kutopokea fedha hizo bandia kwa kuwa watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

“Fedha bandia inafahamika tofauti na fedha halisi kwa hiyo watu waepuke tamaa. Ikibainika mtu ameleta fedha bandia benki atakamatwa ili aeleze ameipata wapi na kama kuna wenzake nao wakamatwe ili sheria ifuate mkondo wake,” alisema Nsekela.

Nsekela alisema wanaongeza umakini kwa kuhakikisha wafanyakazi wao wanafuatilia kuhakikisha fedha zote zinapitia kwenye mashine maalumu kuzuia tatizo hilo ili fedha za wateja zibaki salama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live