Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

BoT yatanga riba elekezi mikopo ya benki

Uchumi Kupanda BoT yatanga riba elekezi mikopo ya benki

Fri, 19 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Benki Kuu Tanzania (BoT) imetangaza riba elekezi ya asilimia 5.5 ya benki kuu kwa benki zote zinazotaka kukopa katika benki hiyo ambayo itakatumika kwa robo ya kwanza ya mwaka 2024 kuanzia leo.

Haya yanajiri baada ya BoT kutangaza kuhama kutoka katika mfumo wa sera ya fedha unaotumia ujazi kuhamia kwenye mfumo wa sera ya fedha unaotumia riba ukiwa na malengo ya kuwezesha ukwasi katika uchumi kuendana na malengo ya kudhibiti mfumuko wa bei na kuwezesha ukuaji wa uchumi.

Gavana Emmanuel Tutuba amesema kiwango hicho cha riba kimezingatia lengo la kuhakikisha thamani ya shilingi dhidi ya fedha za kigeni inaendelea kuwa imara na kinaendana na malengo ya kuhakikisha kuwa mfumuko wa bei unabaki ndani ya lengo la asilimia 5 na kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi kufikia lengo la asilimia 5.5 au zaidi kwa mwaka 2024.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Benki Tanzania (TBA), Geofrey Mchangila amesema hatua hiyo itasaidia pia benki kupanga vizuri viwango vya riba vinavyotolewa na benki nchini licha ya kuwa kiwango cha riba kinaamuliwa na nguvu ya soko.

Mfumo unaotumia riba unatumika katika nchi zote za Afrika Mashariki kama sehemu ya mkakati wa kuwa na sarafu moja na benki kuu moja ya Afrika Mashariki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live