Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

BoT kuleta matawi mikoani

BOT Yaongeza Muda Wa Usimamizi Wa Yetu Microfinance Bank PLC BoT kuleta matawi mikoani

Thu, 18 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya Maendeleo, Dk Ibrahim Mwangalaba amesema wako katika mazungumzo na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ili kupata kibali cha kufungua matawi mikoani kwa mwaka 2024 na kuifanya benki hiyo kuwa ya kitaifa.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Dk Mwangalaba amesema dhamira ni kuifanya benki hiyo kufanya kazi nchi nzima.

“Benki imefikisha mtaji wa Sh bilioni 19 na kuiwezesha benki kufanya kazi nchi nzima na tunapanga kupanua huduma zetu kwa kufungua tawi moja na mawakala wapya 500 ambapo sasa kuna mawakala 1600 zaidi ya mikoa 11" amesema.

Katika hatua nyingine ameeleza kuwa wanatarajia kuanzisha huduma mpya ya kidigitali mwaka huu itakayohusisha utoaji wa mikopo kwa njia ya simu ambapo wateja watapata huduma kwa haraka.

Huduma hiyo mpya ya benki ya mtandaoni (Internet bank) pia itahusisha mfumo wa ukusanyaji malipo ikiwemo ada za shule. -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live