Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

BoT: Wenye hoteli toeni huduma ya kubadili fedha

Dola Dola Juu Juu BoT: Wenye hoteli toeni huduma ya kubadili fedha

Fri, 15 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba amewataka wamiliki wa hoteli zenye hadhi ya nyota tatu mpaka tano nchini kuchangamkia fursa ya kupata leseni kutoka Benki Kuu ya kuanzisha dirisha la kubadilisha fedha za kigeni katika hotel zao ili kusaidia nchi kudhibiti soko haramu la ubadilishwaji wa fedha za kigeni (black market).

Ameyasema hayo jijini Dar es Salaam katika kikao na baadhi ya wawakilishi wa hoteli nchini ambapo ameeleza kuwa utafiti uliofanywa na BoT, ulibaini hoteli nyingi hupokea wateja wanaolipa huduma kwa fedha za kigeni na fedha hizo zinabadilishwa bila kufuata mifumo rasmi ya kubadilisha fedha za kigeni.

Aidha Tutuba ameongeza kuwa ubadilishwaji wa fedha za kigeni kupitia hoteli itarahisisha utoaji wa huduma kwa wageni lakini pia Benki Kuu ambao ndio wasimamizi wa sekta hiyo watapata takwimu halisi za fedha hizo, hatua ambayo itasaidia kudhibiti soko haramu la ubadilishaji wa fedha za kigeni nchini.

Hata hivyo, Gavana ameweka wazi kuwa ili kupata leseni hiyo hoteli hazihitaji kuwa na mtaji wa kuanzisha maduka rasmi kama ilivyo kwenye maduka ya kawaida ya kubadilisha fedha za kigeni huku akisisitiza kuwa hoteli zina jukumu la kutoa huduma kwa shilingi ya Tanzania

Chanzo: www.tanzaniaweb.live