Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

BoT: Uchumi unazidi kuimarika

Uchumi Kupanda BoT: Uchumi unazidi kuimarika

Fri, 9 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa taarifa inayoonesha uchumi wa nchi unazidi kuimarika ikiwa ni pamoja na mauzo ya bidhaa na huduma nje ya nchi kuongezeka kwa asilimia 14.9.

Taarifa ya BoT kuhusu tathmini ya hali ya uchumi kwa mwezi Julai mwaka huu inaonesha katika mwaka ulioshia Juni, 2024, mauzo ya bidhaa na huduma nje ya nchi yalifikia Dola za Marekani milioni 14,680.7.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya kila mwezi fedha hizo zilizotokana na ongezeko la safari, mauzo ya dhahabu, bidhaa za asili, za mbogamboga na matunda.

BoT imeeleza mauzo ya bidhaa za asili nje ya nchi yalifikia Dola za Marekani milioni 1,066.3 likiwa ni ongezeko la asilimia 41.8 kulinganisha na mauzo ya mwaka ulioishia Juni 2023. Taarifa ilieleza ongezeko hilo lilitokana na kiwango kikubwa cha mauzo ya korosho, pamba na kahawa.

BoT ilieleza katika mwaka ulioshia Juni, 2024 mauzo ya tumbaku nje ya nchi yaliongezeka kwa asilimia 140 kutokana na ongezeko la kiwango na bei ya zao hilo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo mauzo ya bidhaa zisizo za asili nje ya nchi yaliongezeka na kufikia Dola za Marekani milioni 6,371.6 kutoka Dola za Marekani milioni 6,195.7 za mwaka ulioshia Juni, 2023.

BoT ilieleza ongezeko hilo lilitokana na mauzo ya dhahabu Dola za Marekani milioni 3,121.8 zikiwa ni sawa na asilimia 49 ya mauzo ya bidhaa zisizo za asili nje ya nchi, bidhaa za matunda na mbogamboga, za samaki na mbegu za mafuta.

Taarifa ilieleza katika kipindi hicho, mauzo ya mbogamboga na matunda yaliongezeka hadi Dola za Marekani milioni 415.4 kutoka Dola milioni 294.1 za mwaka uliopita na ongezeko hilo lilitokana hasa na mauzo ya mbogamboga nje ya nchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live