Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

BoT: Tunataka benki zikopeshe kwa riba asilimia 9

Riba Viwango BoT: Tunataka benki zikopeshe kwa riba asilimia 9

Wed, 23 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema lengo lake ni kuona taasisi za kifedha ikiwemo benki zinatoa mkopo kwa wananchi kwa riba isiyozidi asilimia 9.

Kauli hiyo imetolewa jana Jumanne Novemba 22, 2022 na Gavana wa BoT, Profesa Florens Luoga kwenye kongamano la uwasilishaji wa machapisho ya wataalam wa fedha kuelekea mahafali ya kwanza ya Chuo cha Benki Kuu Tanzania yanayotarajiwa kufanyika Ijumaa ya Novemba 25, 2022.

Amesema agizo la Rais Samia Suluhu Hassan alilolitoa kwenye uzinduzi wa jengo la BoT mkoani Mwanza Juni 13, 2021 akiitaka beni hiyo kuhakikisha riba katika taasisi za kifedha ikiwemo mabenki inashushwa yametekelezwa kwa hadi sasa benki nchini zinatoa mkopo kwa riba ya kati ya asilimia 11 na 13.

Amesema BoT pia imepunguza gharama za uendeshaji wa benki nchini kutoka asilimia 70 hadi 50 na kuanzisha mfuko maalum wa kukopesha mabenki kwa sharti la kukopesha fedha kwa watu kwa riba isiyozidi asilimia 10 huku akisema lengo la kufanya hivyo ni kufikia riba ya dijiti moja.

Wanafunzi 36 kati ya 41 wanatajiwa kuhitimu katika mahafali ya kwanza ya chuo hicho kwenye kozi mbalimbali za uongozi na usimamizi wa fedha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live