Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

BoT, TCRA na TRA hivi hizi Taasisi za Mikopo ya Online zipo kisheria na zinalipa kodi?

Online Loan.png BoT, TCRA na TRA hivi hizi Taasisi za Mikopo ya Online zipo kisheria na zinalipa kodi?

Thu, 23 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kama mnavyojua changamoto zipo kwa Kila mtu hasa upatikanaji wa fedha pale unapokuwa umepata shida ya ghafla yenye uhitaji wa pesa au changamoto kwenye Biashara, mara nyingi unatafuta sehemu kama kwa mtu binafsi au taasisi yoyote ya kifedha ili kupata hela na kutatua tatizo lako.

Kuna taasisi zinazo toa MIKOPO kupitia Mtandaoni ambazo unapakua Application kwenye simu yako kutoka kwa Google unaweka taarifa zako na wanakupa mkopo wa haraka. Sasa malalamiko yangu au pengine kwa niamba ya Watanzania wengine ni kama ifuatavyo;

1. Riba wanazotoza ni kubwa sana wakati wa kurejesha tofauti na maelezo ya hawali, yaani unaweza kuambiwa ukichukua 100,000 unarejesha 130,000 ndani ya wiki moja lakini wakati wa kurejesha unaambiwa rejesha 185,000, huu ni wizi wa hali juu.

2. Unaweza kurejesha hiyo hela lakini hawakufuti kwenye mifumo yao wataendelea kukusumbua wakidai haujalipa.

3. Taratibu za kumdai mteja siyo nzuri kwanza hawana customer care wanatunia kauli mbaya za udhalilishaji pamoja na matusi.

OMBI LANGU 1. Naomba nyinyi kama kama nyinyi wa habari tusaidie kwanza kujua kama hizi taasisi zinazotoa MIKOPO MTANDAONI zimesajiliwa na zinatoa MIKOPO kwa kufuata Sheria, kanuni na Taratibu.

2. Tusaidie kupaza sauti ili kama taasisi hizi zipo kihalali basi ziweke riba halisia ambayo mteja anaweza kumudu na isijekuwa kama ile MIKOPO tunayosika KAUSHA DAMU.

3. Waajiri Wafanyakazi wenye weredi na mafunzo ya huduma kwa mteja (Customer care)

Note: kwa ufuatiliaji naomba nizitaje chache; 1. SINGULARITY MICROFINANCE LTD - kwenye Mtandao (play store au app store wakitumia "Mkopo wako"

2. TEMERIA MICROFINANCE LTD - kwenye mtandao (play store au app store wakitumia " Zima Cash"

Hizo ni chache lakini zipo nyingi sana

Tunaomba Beki Kuu ya Tanzania (BOT), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na taasisi zinazo husika kufuatilia na ikiwezekana kutoa muongozi kama taasisi hizo za kukopesha zinalipa kodi na masharti yao yameridhiwa na mamlaka husika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live