Kamati ya Sera ya Fedha (MPC) ya Benki Kuu imebaini kuwa mfumuko wa bei kwa Tanzania Bara umepungua na kufikia asilimia 3.3 kwa mwezi Septemba 2023 kutoka asilimia 3.6 mwezi Juni mwaka huu ukichangiwa na kupungua kwa bei za vyakula.
Kamati ya Sera ya Fedha (MPC) ya Benki Kuu imebaini kuwa mfumuko wa bei kwa Tanzania Bara umepungua na kufikia asilimia 3.3 kwa mwezi Septemba 2023 kutoka asilimia 3.6 mwezi Juni mwaka huu ukichangiwa na kupungua kwa bei za vyakula. Hata hivyo, kamati imebaini kuwa uchumi wa dunia bado haujaimarika licha ya ukuaji wa juu ya matarajio uliofikiwa katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka.