Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

BoT: Faini milioni 20 kukopesha fedha bila mpangilio

Pic Fedha Data Wastaafu BoT: Faini milioni 20 kukopesha fedha bila mpangilio

Fri, 23 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imepiga marufuku taasisi, kampuni na watu binafsi kufanya biashara ya kukopesha fedha bila kuwa na leseni ya BoT au taasisi zilizokasimishwa majukumu hayo.

Wasiotii sheria inayowataka kuwa na leseni watakabiliwa na kifungo jela kisichozidi miaka miwili au kulipa faini. Imesema ni makosa kisheria kujihusisha na biashara ndogo ya huduma za fedha bila kuwa na leseni ya benki hiyo au taasisi zilizokasimishwa majukumu hayo.

Kupitia taarifa yake kwa umma, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Emmanuel Tutuba alisema benki hiyo imebaini kuwepo kwa baadhi ya taasisi, kampuni na watu binafsi kujihusisha na biashara ya kutoa mikopo bila kuwa na leseni. Alisema jambo hilo ni kinyume na Kifungu cha 16(1) cha Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018.

Tutuba alisema taasisi, kampuni na mtu binafsi wasio na leseni hawaruhusiwi kufanya biashara ya kukopesha na kwamba hatua zitakazochukuliwa kwa ukiukaji wa sheria hiyo ni pamoja na faini isiyopungua Sh milioni 20 au kifungo cha muda usiopungua miaka miwili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live