Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko amewataka Wachimbaji wa Makaa ya mawe na wadau wenye wateja wa bidhaa hiyo kutoka nje kuitumia Bandari ya Mkoani Mtwara katika kuyasafirisha.
Biteko ametoa wito huo, wakati alipotembelea na kuzungumza na uongozi wa bandari ya Mtwara, ili kujionea shughuli zinazofanywa hususan katika usafirishaji wa makaa ya mawe kwenda nje ya nchi.
Amesema, miundombinu katika bandari ya Mtwara inaendelea kuboreshwa ili kuhakikisha makaa ya mawe yanafika kwa wakati nje ya nchi yalipo masoko ya uhakika ya bidhaa hiyo.
Dkt. Biteko ameongeza kuwa, biashara ya makaa ya mawe imekuwa kubwa kutokana na uhitaji wa makaa hayo duniani hali iliyopelekea Bandari ya Mtwara kufanya shughuli nyingi za usafirishaji wa makaa hayo nje ya nchi.