Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Biteko awaka upigaji mrabaha ushuru wa gesi

Tanzania Itaenzi Umoja Wa Bara La Afrika   Biteko.png Biteko awaka upigaji mrabaha ushuru wa gesi

Wed, 15 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Doto Biteko ameagiza vijiji vinavyochimbwa gesi asilia kurejeshewa mrabaha utokanao na ushuru wa gesi ili kuboresha shughuli za maendeleo katika vijiji hivyo ambavyo vimekuwa vikililia changamoto mbalimbali.

Akizungumza katika kijiji cha Msimbati Halmshauri ya Wilaya ya Mtwara amesema kuwa zaidi ya Sh1.5 bilioni zimekuwa zikikusanywa kama ushuru bila fedha hizo kurudi kuendeleza kijiji husika vya Msimbati na Songosongo.

Amesema kuwa amesikiliza maelezo ya wananchi hao kwa uchungu namna wanavyoishi huku wakilipukiwa na gesi huku wakiwa hawana maendeleo ambapo fedha hizo huishia kwenye Halmshauri.

“Yani sielewi wala haiwezekani wala haiingii akilini watu hawa wakalia kukosa kituo cha afya haiwezekani diwani asimame hapa akalia kituo cha afya na kituo cha Polisi, haiwezekani walalamikie ubovu wa barabara nataka kuwaambia Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara yupo hapa na tunakusanya ushuru wa huduma kutoka kwenye gesi inayotoka msimbati zaidi ya Sh1.5 bilioni,”

“Ni kweli mgawanyo wa pesa hizo unatakiwa kusambazwa kwenye Halmshauri nzima lakini asilmia 40 lazima igawanywe vizuri kwa vijiji husika hata kule Songosogno nimeenda wametenga asilimia 20 ya mapato irudi kwenye kijiji husika mradi ulipo lakini cha ajabu kule songosongo hazifiki zinaishia halmashauri,” amesema Biteko.

Biteko amesema kuwa gesi asilia imekuwa ikitokea katika kijiji hicho pamoja na Songosongo ambayo inendesha mitambo ya umeme kwa asilimia 65 ambayo inatumiwa na Watanzania kwaajili ya umeme lakini vijiji hivyo vimekuwa vikikosa mgao huo.

“Kwakweli haiwezekani lazima hizo fedha wananchi wazione hapa hawa watu wanahitaji gesi iliyopo iwanufaishe tunaposema uchumi wa gesi unabadilisha maisha uanze kwa kubadilisha maisha kuonekana kwa watu wa Msimbati,”

“Unajua hawa watu shule waliyonayo haina maana kampuni inayochimba gesi Mnazibay ya M&P inajenga bweni peke na TPDC inatoa Sh40 milioni pekee kwa mradi huu mkubwa hapana naagiza mkurugeniz TPDC na Diwani na DC kuanzia leo msimamie hili”

“Haiwezekani tuje hapa tumependeza alafu watu wanalia shida ndogo ndogo kituo cha polisi mara barabara hawa watu wanastahili kilichobora zaiid hata kuwawekea taa usiku waoone mnashindwa nini mabilioni ya pesa yanatoka hapa yanaenda nchi nzima lazima tofauti ionekane hapa”

Kiongozi huyo ameongeza kuwa kampuni ya M&P inayochimba Gesi asilia Mnazibay ndio ingekuwa kwao wangefurahi kukaa kubanana malalamiko ya watu wa Msimbati huku akiwaambia wananchi hao ndio walinzi wa bomba likipasuka wanajua kabla yao.

Aidha, ameiagiza TPDC kuweka mpango maalum wa Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kwa Jamii (CSR) katika eneo hilo ili wananchi hao waone faida ya kuwepo kwa miradi kwenye maeneo yao na kuwaelekeza kuwaagiza wajenge kituo cha afya, taa za barabarani na kituo cha Polisi.

Ili kuhakikisha kuwa, Jamii zinazozunguka na miradi ya mafuta na gesi asilia zinafaidika na uwepo wa miradi hiyo, amesema kuwa Serikali itakuja na kanuni zitakazoongoza masuala ya CSR lengo likiwa ni kuhakikisha jamii zinazozunguka miradi ya mafuta na gesi zinanufaika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live