Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Biteko atumia mtindo wa Magufuli kusikiliza kero za wachimbaji wadogo

65735 Pic+bite

Sat, 6 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Shinyanga.  Baadhi ya wadau wa madini mkoani Shinyanga wametoa maoni yao mbele ya Waziri wa Mdini Doto Biteko huku wachimbaji wadogo wakidai kuwa bado hawajawezeshwa ipasavyo.

Wadau hao wametoa maoni yao leo Ijumaa Julai 5, 2019 katika mkutano mkuu mdogo wa wadau wa madini ya Almasi, uliofanyika mkoani Shinyanga.

Hiyo ni baada ya Waziri huyo kuamua kutumia mfumo alioutumia Rais, John Magufuli katika kusikiliza maoni ya wadau hao na kuyafanyia kazi.

Baadhi ya wachimbaji wamesema licha ya kuwa wao ndiyo chanzo cha mapato ya uchimbaji, bado ni duni kwa kukosa vifaa.

Mmoja wa wachimbaji hao, Maige Nese ameiomba Serikali kusimamia sheria ipasavyo ili kila mmoja wao, wakiwamo madalali, watimize majukumu yao.

Kwa upande wake mchimbaji mdogo George Ngasha, aliwasilisha kilio chake kuhusu maeneo ya uchimbaji kuwa ni tatizo na kuongeza kuwa mashimo yao ya uchimbaji yanamilikiwa na migodi mikubwa.

Pia Soma

Ametaja kata ambazo baadhi ya maeneo ya wachimbaji wadogo yamechukuliwa na migodi mikubwa ni Kata ya Maganzo, Songwa, Mondo na Idokilo.

Masanja Meja ambaye ni madalali, ameiomba wizara itoe elimu kwa wachimbaji wadogo n madalali na wauzaji ili kila mmoja aijue nafasi yake.

Kutokana na maoni hayo, Biteko amewahakikishia kuwa maoni yao yote yamechukuliwa na yatafanyiwa kazi kuanzia wiki ijayo.

 Amemuagiza Ofisa Madini Mkazi Mkoa wa Shinyanga, Joseph Kumburu kuandaa kikao  cha wadau hao ili kuanisha yote yaliyoainishwa ili yaliyo chini ya uwezo wake ayatatue.

Chanzo: mwananchi.co.tz