Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Biteko ashiriki mkutano wa mawaziri wa Nishati

Dk. Doto Biteko Wq Dk. Doto Biteko kwenye mkutano.

Thu, 15 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko ameshiriki kikao cha 19 cha pamoja cha Mawaziri wa Nishati ambao ni Wanachama wa Umoja wa soko la pamoja la kuuziana umeme na kuimarisha mifumo ya Gridi ya EAPP unaofanyika nchini Uganda.

Mkutano huo unajadili masuala mbalimbali ikiwemo kupitisha mabadiliko ya mikataba ya uongozi wa EAPP, kuridhia kanuni za uanzishwaji wa kitengo kinachojitegemea cha kusimamia soko la biashara ya umeme kwa nchi wanachama na kuridhia kanuni na taratibu za uendeshaji wa vikao vya Baraza la Mawaziri, Makatibu wakuu, na kamati ya uongozi.

Mkutano huo umehudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Dennis Londo, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Felchesmi Mramba, Mkurugenzi wa Shirika la Umeme (TANESCO), Gissima Nyamo-Hanga, Naibu Mkurugenzi Mipango, utafiti na uwekezaji CPA Renatha Ndege, na viongozi waandamizi kutoka Wizara ya Nishati na taasisi zake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live