Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Biteko asema sekta ya madini imepata ufumbuzi

68569 Pic+biteko

Sun, 28 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Waziri wa Madini nchini Tanzania, Doto Biteko amesema sekta ya madini imekua ikiundiwa kamati nyingi lakini katika Serikali ya awamu ya tano imeamua kutekeleza kwa vitendo mapendekezo yenye tija ili kuhakikisha sekta hiyo inaleta tija kwa wananchi.

Akizungumza jana Jumamosi Julai 27, 2019 katika kongamano la Umoja wa Wanawake (UWT) wa Chama cha Mapinduzi la  kumpongeza Rais wa Tanzania John Magufuli kutekeleza Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya mwaka 2015/20 kuwa sasa hivi madini yanatoa mchango muhimu.

Alisema kabla ya awamu ya tano maeneo yaliyokuwa yametengwa kwa wachimbaji wadogo yalikua 25 nchi nzima sasa hivi yapo maeneo zaidi ya 175.

"Wachimbaji wadogo zaidi ya 5,620 nchi nzima wamepewa leseni huku masoko ya madini 28 yamefunguliwa na kiasi cha Sh137 bilioni zimetumika kununua madini katika masoko hayo," alisema Biteko

Biteko aliongeza kuwa ujenzi wa ukuta wa Mirerani wilaya ya Simanjiro Mkoa wa Manyara umeongeza kiwango cha mapato kwa Serikali ya Tanzania kutoka Sh167 milioni hadi Sh2.8 bilioni.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha alisema kiwango cha urejeshaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu imeongezeka na kwamba asilimia 40 ya fedha zinazotolewa kama mikopo inatokana na marejesho hayo.

Pia Soma

Alisema mwaka 2019 wanafunzi wapatao 128,000 watanufaika na mikopo ya elimu ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi huku Sh2.9 bilioni zimetumika kujenga shule ya elimu maalumu ya Patandi wilayani Arumeru mkoani Arusha itakayopokea wanafunzi wenye ulemavu nchini.

Ole Nasha alisema Serikali imekua ikitoa Sh24 bilioni kila mwezi ili kuwezesha elimu bure katika shule za msingi na sekondari.

Chanzo: mwananchi.co.tz