Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Biteko aitaka Barrick Goldmine kuwekeza bila uoaga

0bb8abe5faa5dc301ace6d04b465cc0b Biteko aitaka Barrick Goldmine kuwekeza bila uoaga

Mon, 1 Mar 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WAZIRI wa Madini, Dotto Biteko amesema kampuni ya uchimbaji wa madini ya Barrick Goldmine inatakiwa kuwekeza bila kuogopa chochote bali ihakikishe inazingatia sheria za madini pamoja na sheria za nchi.

Alisema hayo wakati alipokuwa katika mkutano maalumu na watendaji wa mgodi wa Barrick.

“Ninachowambia Barrick wahakikishe wanawekeza nchini kwetu kwa kuzingatia sheria zetu za madini tulizoboresha pamoja na sheria za nchi. Rais wetu amewahakikishia ushirikiano,” alisema Biteko.

Alisema mpaka sasa mgodi huo umeshatoa ajira zaidi ya 42,000 kwa Watanzania na kuupongeza mgodi huo kwa kuendelea kufanya kazi hapa nchini.

Alisema mgodi huo umetoa dola ya Marekani zaidi ya milioni 290 kwa ajili ya malipo mbalimbali katika kampuni za ndani.

Mkurugenzi Mtendaji wa mgodi Barrick, Mark Bristow alisema wataendelea kufanya kazi zao za uchimbaji katika migodi ya (North Mara, Bulyanhulu and Buzwagi) kwa kuendelea kufuata utaratibu wote na sheria za nchi.

Alisema wamekuwa wakishirikiana na jamii za mitaa kurejesha leseni ya kijamii ya migodi kufanya kazi na wanashirikiana kwa karibu na mamlaka husika katika masuala ya mazingira North Mara.

Chanzo: habarileo.co.tz