Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Biteko ahimiza AU kuongeza kwenye miradi ya PIDA

Biteko Awataka Wafanyabiashara Wa Madini Kurejesha Fedha Za Kigeni Biteko ahimiza AU kuongeza kwenye miradi ya PIDA

Fri, 15 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri Mkuu na waziri wa Nishati wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Dotto Biteko amesema upo umuhimu kwa nchi za Afrika kufanya juhudi za utafutaji wa rasilimali fedha kwaajili ya kuongeza kasi katika miradi ya Mapango wa maendeleo ya miundombinu ya Afrika (PIDA)

Dkt. Biteko ameeleza hayo katika hotuba aliyoisoma kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi wakati wa ufungaji wa mkutano wa nne wa mawaziri wa sekta ya uchukuzi, miundombinu na Nishati wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika uliofanyika kwa siku nne visiwani Zanzibar

Amesema pamoja na mambo mengine pia nchi wanachama kwa kushirkiana kwa pamoja wanawajibu wa kuboresha upatikanaji wa huduma za nishati barani Afrika kwani bado kuna changamoto licha ya kuweko kwa utajiri mkubwa wa raslimali za nishati Afrika

Chanzo: www.tanzaniaweb.live