Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Biteko: Rais anataka mahusiani mazuri TRA, wafanyabiashara

Rais Samia Anatamani Mradi Wa JNHPP Uanze Haraka   Dkt. Biteko Biteko: Rais anataka mahusiani mazuri TRA, wafanyabiashara

Sat, 25 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amewataka Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mamlaka ya Mapato Tanzania – TRA, kuhakikisha kuwa wanatekeleza agizo la Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan la kuendelea kutoa elimu ya mlipakodi kwa Watanzania na Wafanyabiashara ili kuleta ufanisi katika ukusanyaji kodi, kuendelea kuweka uhusiano mzuri kati ya Wafanyabiashara na TRA na kuhakikisha kuwa kila anayestahili kulipa kodi nchini, anailipa bila misukosuko.

Dkt. Biteko amesema hayo wakati alipokuwa mgeni rasmi katika Sherehe ya utoaji Tuzo kwa Walipakodi Bora kwa mwaka 2022/2023 iliyofanyika tarehe 24 Novemba, 2023 jijini Dar es Salaam.

Amesema, “Wafanyabiashara wanapaswa kulelewa ili walipe kodi zaidi, wanapaswa kufundishwa umuhimu wa kulipa kodi, na kazi hii ni ya kwenu Wizara ya Fedha na TRA na ninafurahi kwamba mnaifanya vizuri, sisi tunawatakia kila la heri katika kuifanya kazi hiyo ili mchango wa walipa kodi uendelee kuwa mkubwa ili tuweze kufikia malengo tunayojiwekea.”

Dkt. Biteko aliipongeza TRA kwa kusimamia vizuri zoezi la ukusanyaji mapato nchini akitolea mfano malengo waliyowekewa mwaka 2022/23 ambayo wameyafikia kwa asilimia 97.4 kwani walikusanya shilingi Trilioni 24.11 kati ya shilingi Trilioni 24.76 walizopangiwa na kueleza kuwa hiyo si hatua ndogo hivyo TRA na Walipakodi wote wanastahili pongezi.

Amewataka Wafanyabiashara kutambua kuwa, kazi ya kujenga nchi si ya Serikali pekeyake bali ni ya watanzania wote hivyo amewataka kuendelea kulipa kodi ili zikajenge nchi kwa namna mbalimbali ikiwemo ujenzi wa Barabara, Shule, Umeme, Maji, Hospitali zenye madawa na nyenzo nyingine ambazo uwepo wake unahitaji fedha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live