Waziri Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanapanda miti kwa wingi hasa katika kipindi hiki cha mvua ili iweze kukua na kuingia katika biashara ya kaboni.
Waziri Chana, ameyasema hayo wakati wa hafla ya hafla ya kusaini hati ya makubaliano kati ya kampuni hiyo na Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), kuhusu biashara ya kaboni, na kudai kuwa Tanzania ina eneo la takriban hekta milioni 48.1 zenye misitu, ambayo ina faida nyingi kwa wananchi.
Tetemeko la ardhi Uturuki, Watanzania wapo salama: BaloziAmesema, “Tukitunza misitu yetu tutapata faida nyingi kwan tunaona vyanzo vya maji vinategemea misitu, sekta nyingi zinategemea miti mfano kilimo, afya, ujenzi, mindombinu hivyo ni kuhimu kulinda kuhifadhi misitu.”
Taasisi hiyo ya Blue Carbon UAE na Serikali ya Tanzania kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), zimetia saini mkataba wa makubaliano kuanza kwa ushirikiano wenye lengo la kukuza usimamizi endelevu wa misitu na kupunguza ukame.