Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Binti, anza na biashara hizi baada ya kumaliza chuo

Biashara Zxc Binti, anza na biashara hizi baada ya kumaliza chuo

Thu, 18 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maisha ni mapambano na kila siku tunaamka kupambana, mkono uende kinywani. Wanawake pia wamekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya familia. Ni ukweli kwamba baba ni kichwa cha nyumba na kwa tamaduni zetu za Africa ni ‘mtafuta mkate namba moja’. Ila mama ni msaidizi sana pia.

Kuna familia nyingine mama ni nguzo kuu. Labda alifiwa na mume wake aliyekuwa tegemezi na ikambidi asimame kwa ajili ya kuwalea watoto wake. Lakini wengine walitelekezwa na watoto na hawakurudi nyuma wakaendelea kupambana wenyewe.

Katika dunia ya leo bidhaa zimekuwa nyingi duniani na hata hapa nyumbani Tanzania. Kuna wakati katika safari zangu napita barabara ya Kilwa Road hapa Dar es Salaam na hua natazama sana wanawake wanavyofanya biashara mbalimbali maeneo ya Mbagala Rangi Tatu.

Utamuona huyu amekaa na mtoto wake mdogo na beseni lake lililojaa matunda ukitazama mtaji wake unaweza usifike hata elfu ishirini.Lakini ameamua kutoka na kutafuta riziki yake. Wanawake wengine utawaona wanatembea wakiwa wameshika mkono huu chumvi za jikoni na mkono mwingine sumu au dawa za kuchoma za mmbu. Yote ni katika kupambana.

Ukiingia katika mitandao ya kijamii pia wanawake wengi wanajituma sana. Biashara za Online zimekuwa mkombozi wa wasichana wengi mathalani kuna mabinti wengi wamemaliza chuo hawajapata ajira na wakaamua kujiajiri katika biashara mbalimbali mfano kuuza vipodozi vya urembo, kashata,korosho,nguo na vitu vingine.

Katika video huyu ni Sue Owino kutoka Kenya amejikita katika kutengeneza maudhui mtandaoni upande wa chakula fursa anazopata ni kupata matangazo ya chakula na vinywaji kutoka kampuni mbalimbali na kujiingizia kiapato.

Fanya hivi kama una mtaji mdogo;

Nunua vitu kama nguo za ndani,cheni, au hereni nenda Kariakoo kwa wale wa Dar, zipige picha vizuri kisha weka katika mtandao wa kijamii kama Whatsapp au Facebook kwa ajili ya kutafuta wateja.

Nenda Kariakoo ingia kwenye duka unalohitaji bidhaa fulani ya kuuza na pesa ni ndogo omba kupiga picha (mara nyingi hawakatai) bidhaa zao kisha post kwenye mtandao wa kijamii kama umeambiwa aina fulani ya nguo labda ni elfu thelathini ongeza na faida yako toa bei.

Kama unapenda mapishi na nyumbani kuna jiko kwa ajili ya keki (oven) unaweza kuanza kujifunza kupitia youtube na kutengeneza vitu kama cookies na biskuti kisha kuomba maduka ya jirani kuuza bidhaa zako.

Pia unaweza kuamua kuanza kutengeneza juisi nyumbani kama kuna kifaa cha kusagia kama hakuna unaweza kununua ya bei ndogo.

Tafuta soko linalouza matunda ya bei rahisi kama Stereo Temeke, Ilala sokoni, mabibo au buguruni kwa wale wa kazi wa Dar.

Tengeneza kwa usafi weka kwenye dumu peleka kituo cha bodaboda au sokoni uza.

Uza ubuyu, uza kashata biashara hizi unaweza ukaanza kuuza kwa wanafamilia katika group la Whatsapp au magroup mengine ya shule na kadhalika.

Utunzi wa Maudhui (Content Creating); hii imekuwa njia ya kupata kipato mitandaoni na unaweza ukaanza kwa kutumia smartphone yako na kutafuta maudhui watu wanayoweza kuyapenda.

Hakikisha unatengeneza ukurasa mzuri katika mtandao wa kijamii utakaochagua.

Biashara hazitakiwi uoga ni vyema kujua malengo yako na unataka ufanikiwe kwa namna gani.

Waswahili wanasema ukizaliwa peke yako na utakufa peke yako ni vyema kuchanganua namna utakayoweza kupata kipato bila uoga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live