Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bilioni 73/- kuimarisha usafiri wa anga Mtwara

Pesa Fedhaddd Bilioni 73 kuimarisha usafiri wa anga Mtwara

Tue, 30 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SERIKALI imeisaini mkataba wa Sh bilioni 73.5 kwa ajili ujenzi wa jengo la abiria, vituo vya zimamoto, Hali ya hewa pamoja na mnara wa kuongozea ndege katika kiwanja cha ndege cha Mtwara.

Mkataba huo umesainiwa kati ya Mkurungezi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Tanzania (TAA) Ibrahim Mbura na Mkandarasi wa China Railway Engineering Company Group.

Hafla ya utiaji saini imeshuhudiwa na Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala na viongozi wengine wa kitaifa wakiwemo wabunge. Hafla hiyo imefanyika katika uwanja mpya wa Ndege Mkoani humu.

Akizungumza katika hafla hiyo, Profesa Mbarawa amesema fedha ya utekelezaji wa mradi ipo tayari na kwamba tayari Mkandarasi yupo saiti kwa ajili ya utekelezaji wa mradi.

"Mkandarasi ana uwezo mkubwa na hatuna shaka kazi itamalizika kwa viwango na kwa wakati uliopangwa," amesema na kuongeza kuwa mradi huo utatekelezwa kwa muda wa miezi 36.

Mkuu wa Mkoa Kanali Patrick Sawala ameishukuru wizara ya Uchukuzi kwa kuendelea kutekeleza maagizo ya Raisi Dkt Samia Suluhu Hassan kuhusu ujenzi wa miradi ya maendeleo Mkoa wa Mtwara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live