Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bilioni 71.5/- zatolewa mikopo kilimo biashara

Prof.RaphaelChibunda And Mr. Nicomed Bohay Bilioni 71.5/- zatolewa mikopo kilimo biashara

Wed, 15 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KILIMOBIASHARA nchini kinaendeshwa kwa kiwango kikubwa kupitia uwezeshaji wa asasi inayoitwa Private Agricultural Sector Support (PASS) Trust, Mkurugenzi wake, Nicomed Bohay, anasema.

Katika kipindi cha wiki mbili zilizopita, asasu hiyo imekuwa ikiwakutanisha viongozi na wadau mbalimbali nchini kuzungumzia mipango mikakati ya kuinua wajasiriamali ambao wanahitaji uwezesho wa kifedha.

“Kuanzia Januario hadi Machi mwaka huu, tumewezesha upatikanaji wa mikopo yenye thamani ya Sh. bilioni 71.5 tukitumaini kuwa wajasirimali kupitia kilimobiashara watashiriki zaidi na kuongeza uzalishaji wa bidhaa, alisema Bohay jijini Mbeya.

Alisema kuwa tangu kuanzishwa kwake mwaka 2000, PASS imekuwa na mchango mkubwa katika uchumi na kilimo, ikisaidia wajasiriamali kunufaika na mikopo kutoka taasisi za fedha, sasa wakishirikiana na taasisi 16 zikiwamo benki.Alisema wajasirimali wanawake wana manufaa zaidi wakipata asilimia kati ya 60 na 80 ya udhamini wa PASS katika mikopo ya benki wakiwa kwenye ama vikundi vya wakulima au mkulima mmoja mmoja.

Kiongozi huyo alisema PASS inatoa huduma mbalimbali za maendeleo ya biashara zikiwamo tathmini, maendeleo ya mpango wa biashara na mafunzo kwa makundi ya wakulima.Akizungumza katika mkutano wa wadau jijini Mbeya, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, aliipongeza PASS Trust kwa kuwawezesha wakulima kuzifikia huduma za kifedha na kuwa na uhakika wa kushiriki kikamilifu katika kilimo.

"Wajasiriamali katika kilimobiashara mkoani hapa wachangamkie fursa ya huduma za PASS kuboresha maisha yao. PASS imerahisha njia kwa kila mmoja wakiwamo vijana kushiriki katika kilimobiashara na kutengeneza ajira," alisifu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live