Halmashauri ya Jiji la Tanga inatarajia kutumia kiasi cha Sh bilioni 7.7 kwa ajili ya kujenga soko la Kudumu ambalo litatumika na wafanyabiashara wadogo maarufu Machinga.
Akiongea wakati wa ziara yake ya kukagua Maendeleo ya ujenzi wa soko hilo Mkuu wa wilaya ya Tanga, Hashim Mgandilwa amesema kuwa kukamilika kwa soko hilo kutawasaidia wafanyabiashara hao kuwa nauhakika wa eneo ambalo wataweza kufanya shughuli zao Kila siku.
"Tunatakribani wamachinga 900 ambao kwa Sasa wanafanya shughuli zao Kwa siku maalum katika eneo ambalo sio rasmi la Tangamano lakini hapa Sasa watakuwa na soko rasmi"amesema DC Mgandilwa.
Mkurungenzi wa Jiji la Tanga Sipora Liana amesema kuwa soko hilo litajengwa kwa kupitia fedha kutoka serikali kuu pamoja na mapato ya ndani .