Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bilioni 50 zatengwa nishati ya gesi

Gesiii Bilioni 50 zatengwa nishati ya gesi

Tue, 19 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Nishati, Januari Makamba amesema serikali imetenga Sh bilioni 10.5 kwa ajili ya uwekezaji wa nishati ya gesi ili kuondokana na matumizi ya mkaa na kuni.

January alisema hayo jana wilayani Kahama mkoani Shinyanga baada ya kutembelea Shule ya Sekondari Queen of Family yenye mradi wa gesi kwa ajili ya kupikia.

Alisema Sh milioni 500 zimetengwa kwa ajili ya uhamasishaji wananchi ili waaache kutumia kuni na mkaa.

"Kila mwaka watu 22,000 kupoteza maisha kutokana na madhara ya matumizi ya mkaa na kuni kwa kusababu ya moshi unaotoka wenye sumu ya carbomonoxide katika mkaa hivyo serikali inataka kuvidhibiti vifo vinavyotokana na suala hilo," alisema January.

Alisema Sera ya Nishati ya mwaka 2015 inasema kila mtu atatumia nishati ya gesi ili kuondokana na matumizi ya mkaa au kuni na serikali itapita kila eneo lenye mradi ili kuboresha mapungufu yaliyopo.

January alisema amefanya ziara hiyo ili kuona miradi ya gesi kama ipo imara na kuhakikisha nishati ya umeme inapatikana kwa uhakika katika maeneo ya viwanda, taasisi na majumbani.

Mwalimu wa taaluma kutoka shule hiyo, Hezekia Mafuru alisema walianzisha mradi wa gesi mwaka 2011 kwa ajili ya kupikia na kwamba imewapatia manufaa kwa sababu ni somo ambalo wanafunzi wanalisoma kwa vitendo hasa wa masomo ya fizikia na kemia.

Shule hiyo ambayo kwa sasa hawatumii mkaa na kuni ilianzishwa mwaka 2006 na ina wanafunzi 368

Chanzo: www.tanzaniaweb.live