Katika kuongeza kasi ya upatikanaji umeme nchini tumepanga kutekeleza Mradi wa Kuzalisha Umeme Jua Mkoani Shinyanga wa MW 150.
Mradi huu unahusu ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia jua katika eneo la Kishapu mkoani ambapo gharama ya mradi huu ni Euro milioni 115.30 sawa na Shilingi bilioni 294.02 kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo ya Ufaransa (AFD).
Mradi huu unatekelezwa katika awamu mbili, ambapo awamu ya kwanza itahusu ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa MW 50 utakaogharimu Shilingi bilioni 109.65 na awamu ya pili itahusisha ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme wa MW 100 utakaogharimu Shilingi bilioni 184.37