Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bilioni 20/- kuboresha mabwawa ya umeme

Bwawa La Umeme Nyerere 780x470 1 Bilioni 20/- kuboresha mabwawa ya umeme

Mon, 11 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SERIKALI imetoa Sh bilioni 20 zitakazotumika kuboresha miundombinu ya kuzalishia umeme katika bwawa la Mtera, Kidatu na Kihansi.

Kati ya fedha hizo, Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga alisema Sh bilioni 8 ni kwa ajili ya Kihansi, Sh bilioni 4, Mtera na Sh bilioni 8 zinazobaki zimetengwa kwa ajili ya Kidatu.

"Mbali na fedha hizo za maboresho, niwahakikishie watanzania kwamba vyanzo vyetu vya umeme nchini vinafanya kazi kwa ufanisi mkubwa, kwahiyo wasiwe na shaka," alisema.

Alisema yeye pamoja na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Nishati na Madini wamejionea jinsi kituo cha kuzalisha umeme cha Kihansi kinavyotumia teknolojia ya kisasa kuzalisha megawati 180 ya nishati hiyo.

"Tunamshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyopambana kuhakikisha vituo hivi pamoja na mradi mkubwa wa Mwalimu Nyerere unamaliza changamoto ya umeme iliyokuwa ikijitokeza huko nyuma," alisema.

Alisema Februari 2024 serikali inatarajia kufanya majaribio ya uzalishaji wa umeme katika bwawa hilo la Mwalimu Nyerere kabla ya kuzindua rasmi uzalishaji wake itakapofika Juni, 2024.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live