Serikali kupitia Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imetenga kiasi cha Shilingi Bilioni 2 kupitia mapato ya ndani kwa ajili ya kuanza ujenzi wa stendi y amabasi yaendayo mikoa ya kusini katika eneo la Mbagala jijini Dar es Salaam.
Serikali kupitia Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imetenga kiasi cha Shilingi Bilioni 2 kupitia mapato ya ndani kwa ajili ya kuanza ujenzi wa stendi y amabasi yaendayo mikoa ya kusini katika eneo la Mbagala jijini Dar es Salaam. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Deogratius Ndejembi kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI) bungeni mjini Dodoma leo kufuatia swali lililoulizwa na Abdallah Jafari Chaurembo, Mbunge wa Jimbo la Mbagala kuhusu ujenzi wa stendi hiyo.