Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bilioni 2.8 zatolewa kwa wajasiriamali Tanga

Bilioni 2.8 Zatolewa Kwa Wajasiriamali Tanga Bilioni 2.8 zatolewa kwa wajasiriamali Tanga

Mon, 31 Oct 2022 Chanzo: Eatv

Halmashauri ya Jiji la Tanga imefanikiwa kuongeza kiwango cha utoaji wa fedha za mikopo kwa vikundi vya kiuchumi vya wanawake, vijana na wenye ulemavu kutoka katika asilimia kumi (10%) ya mapato yake ya ndani, ambapo kwa mwaka wa fedha 2021/2022 jumla ya shillingi Billion 2,088,530,000.00

Kiwango hicho cha fedha, kinajumuisha fedha zilizopangwa kutoka Bajeti ya mapato kwa mwaka huo, kiasi cha Billion 1,115,607,800.00 pamoja na fedha za marejesho ambazo nazo zimeingia katika mzunguko wa ukopeshaji.

Akikabidhi mfano wa hundi zenye thamani ya shillingi million 377 kwa vikundi 43 (Wanawake vikundi 31 wakipokea jumla ya shillingi million 266, Vijana vikundi 6 Tsh. 83 M na wenye ulemavu vikundi 6 Tsh. 28 M), ambapo vinahitimisha awamu ya nne ya utoaji kwa mwaka 2021/2022.

Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdulrahman Shiloow amewataka wanavikundi hao kuzingatia mipango yao na kufanya biashara zenye tija ili warudishe mkopo na kupata faida ya kazi na kubadili hali zao za maisha.

Amesema fedha hizo sio za bure, ni mkopo, hivyo wanapaswa kufanya utafiti wa biashara sio kuiga kwa mwingine.  

Chanzo: Eatv