Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bilioni 2.17 kuinufaisha Tanzania kupitia Bahari ya Hindi

Eae3a06a2d37d87ac9b760669e2db65d.jpeg Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah

Sun, 15 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tanzania inatarajia kupata Euro Milioni 2.17 sawa na Shilingi za Kitanzania Bilioni 5.2 kwenye mradi wa uhifadhi wa bainuai za Bahari ya Hindi na maeneo Tengefu ya Ukanda wa Pwani.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah katika mazungumzo yake na ujumbe kutoka Ubalozi wa Ujerumani hapa nchini na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) na kufanya mazungumzo ya kukazia ushirikiano baina ya Tanzania na Ujerumani, kwenye uhifadhi wa bainuai za Bahari ya Hindi na maeneo Tengefu ya Ukanda wa Pwani.

“Huu mradi una faida unalenga kuhifadhi bainuai, utatoa elimu kwa jamii inayokaa katika maeneo hayo na tunategemea mradi utafanya rasilimali kuwa endelevu kwa muda mrefu na utaongeza kipato kwa wananchi, kwa kuwa wataelimishwa njia mbadala za maisha na kuhifadhi maeneo Tengefu.” Amesema

Naye Mkuu wa Ushirikiano wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Ujerumani hapa nchini Dkt. Katrin Bornemann amesema ana furaha kwamba ushirikiano baina ya Ujerumani na Tanzania katika maeneo ya bainuani na maeneo Tengefu utakuwa na nguvu katika kuhakikisha Ukanda wa Pwani wa Bahari ya Hindi unatunzwa pamoja na kuhakikisha rasilimali zilizopo katika maeneo Tengefu zinaendelezwa.

Kwa upande wa Mratibu wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) nchini Tanzania Ralf Senzel, amesema mradi huo utajenga uhusiano mzuri baina ya nchi hizo mbili.

Mazungumzo hayo baina ya Katibu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah na Mkuu wa Ushirikiano wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Ujerumani hapa nchini Dkt. Katrin Bornemann pamoja na Mratibu wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) nchini Tanzania Ralf Senzel, yamehudhuriwa pia na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Dkt. Ishmael Kimirei, Kaimu Meneja wa Kitengo cha Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) John Komakoma ambapo mradi huo utatekelezwa na Mratibu wa Usimamizi Shirikishi wa Rasilimali za Uvuvi Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi (SWIOFish) Dkt. Nichrous Mlalila.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live