Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bilioni 13 kuendeleza bonde la ziwa Victoria

9a6f674d5eb0399dbde97e202a34a4ff Liberata Mulamula wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Wed, 1 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeratibu na kufanikisha upatikanaji wa Euro milioni 5.3 kupitia Programu ya Pamoja ya Usimamizi na Uendelezaji wa Rasilimali za Maji katika Bonde la Ziwa Victoria.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika mashariki, Balozi Liberata Mulamula amesema hayo bungeni mjini Dodoma alipokuwa akiwasilisha bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 20222/2023.

Balozi Mulamula amesema fedha hizi zitaiwezesha Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza kukarabati na kupanua mtandao wake wa majitaka kwa kilomita 14.4, kuunganisha kaya 1,600 kwenye mtandao huo na kununua vifaa.

Waziri Mulamula ameliambia Bunge kuwa programu hiyo inaratibiwa na kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria ya Afrika Mashariki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live