Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bilionea awakatia ndege wake 80 tiketi za ndege

Falcon Ndege.jpeg Bilionea awakatia ndege wake 80 tiketi za ndege

Sat, 15 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mfanyabiashara Ahmet Yasar mwenye makazi yake huko Uturuki aliingia katika gumzo mitandaoni baada ya kukata tiketi za ndege 80 kwa ajili ya kusafirisha ndege wake kuelekea Jeddah huko Saud Arabia.

Picha zilisambaa kwa kasi baada ya kuchapishwa kwenye mtandao wa Reddit zikiwaonesha ndege hao wakiwa kwenye usafiri wa ndege za kampuni ya Emirates.

Katika tukio hilo inadaiwa kila ndege mmoja (Falcon) alikuwa na thamani ya takriban shilingi milioni 18 za Tanzania.

“Picha niliyochapisha imeenea sana na kuvutia watu kutoka kote ulimwenguni,” alisema.

Bw Yasar alisema rubani wa shirika la ndege hiyo ndiye aliyepiga picha hizo ingawa hakumtaja jina na kuongeza kuwa ni rafiki yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live