Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bilionea Musk ataka kuinunua Twitter

Elon Mask111.png Bilionea Elon Musk

Thu, 14 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bilionea Elon Musk ameweka dau la Dola za Marekani bilioni 41 ili kununua mtandao wa kijamii wa Twitter, ikiwa ni siku chache zimepita tangu anunue asilimia tisa ya hisa za kampuni hiyo.

“Tangu nimefanya uwekezaji, sasa nimegundua kampuni hii haiwezi kuendelea kukua au kutoa huduma bora kwa jamii ikiwa katika mfumo uliopo hivi sasa, Twitter inahitaji kubadilishwa na kuwa kampuni binafsi hasa,”amesema Musk.

"Ofa yangu ni bora na ya mwisho, na kama haitakubwaliwa, nitafikiria upya nafasi yangu kama mwanahisa,”aliongeza.

Musk ana idadi kubwa ya wafuasi kwenye mtandao huo wanaofikia milioni 80 tangu ajiunge na Twitter mwaka 2009, na amekuwa akitumia mtandao huo kutoa matangazo mbalimbali kuhusu kampuni yake ya Tesla Motors.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live