Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bilionea Laiza aiomba serikali umeme

LAIZER Bilionea Laiza

Mon, 9 Aug 2021 Chanzo: ippmedia.com

Alisema jamii ya wafugaji wa vijiji vya Lengasiti na Olchoronyori wanatumia gharama kubwa kununua mafuta ya kusukuma maji yaliyochimbwa kwenye visima ili kunywesha mifugo yao.

Akizungumza mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Dk. Suleimani Serera, Saniniu, alisema kuna visima vitatu vya maji eneo hilo, lakini hakuna huduma ya nishati ambayo itasukuma maji.

“Kati ya visima vitatu vya maeneo hayo, kimoja kilichimbwa na serikali na viwili nilichimba kwa gharama zangu lakini hakuna nishati ya umeme hivyo serikali itusaidie kupata huduma ya umeme,” alisema bilionea Laizer.

Alisema gharama ya kununua mafuta ya diseli ya kuendesha mitambo hiyo ni kubwa kwa kuwa lita 200 zinatumika na kwa siku mbili  kunahudumia mifugo zaidi ya 10,000.

Hata hivyo, alisema jamii ya wafugaji wa eneo hilo, wanatakiwa kuangaliwa na serikali kwa jicho la huruma kwa kuwa umeme ukiwapo utarahisisha maendeleo yao.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Dk. Serera, alisema serikali itahakikisha eneo hilo linapatiwa nishati ya umeme ili kurahisisha upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi wa eneo hili pamoja na mifugo.

Dk. Serera, alisema serikali itaunga mkono juhudi za wadau wa maendeleo akiwamo bilionea Laizer, kwa kuwa wamekuwa wakitumia fedha zao kwa ajili ya kuinufaisha jamii inayowazunguka.   

Alisema Meneja wa Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilayani humo, Mhandisi Joanes Martin, ni kijana mchapakazi atamwagiza afuatilie suala hilo.

Alisema serikali iliahidi kuwa itahakikisha vijiji vyote vinapatiwa nishati ya umeme, hivyo katika wilaya hiyo watahakikisha maeneo yote yasiyokuwa na umeme yatafikiwa.

Chanzo: ippmedia.com