Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bil 700/-zatengwa bunifu kuwa bidhaa kwenda sokoni

452819f8b8994e62215a4283ece40590 Bil 700/-zatengwa bunifu kuwa bidhaa kwenda sokoni

Mon, 23 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SERIKAli imetenga Sh milioni 700 kwa ajili ya kusaidia kuendeleza bunifu ili ziwe bidhaa na kwenda sokoni.

Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omar Kipanga wakati akifungua mafunzo kwa wabunifu walioshiriki Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu(MAKISATU) mwaka 2022 yaliyoandaliwa na Tume ya Sayansi Teknolojia (COSTECH).

Alisema serikali imetenga Sh milioni 700 kwa ajili ya kusaidia na kuendeleza bunifu ili ziwe bidhaa na kwenda sokoni.

Alisema kuwa serikali imejipanga vizuri kuhakikisha kuwa inazitambua bunifu na kuzipeleka sokoni.

"Tulikuwa kwenye wiki ya MWAKISATU kuanzia Mei 16 hadi 20, baada ya kumalizika kwa mashindano ya wabunifu tukasema tutakaa nao kwa siku tatu ili kuhakikisha wanatengeneza uwezo wa pamoja kwani kubuni ni jambo moja na kutekeleza ni jambo jingine," alisema.

Alisema hata Makamu wa Rais, Dk Phillip Mpango alisisitiza ,vijana, wanafunzi walioibuliwa katika ubunifu kufuatiliwa na kuendelezwa.

Alisema kuwa baada ya wiki ya ubunifu kumalizika walikaa kama wizara na kutenga Sh milioni 700 ambazo zitasaidia kuendeleza bunifu na tayari wamepata wafadhili mbalimbali wa kuwaunga mkono.

Alisema kuwa Shirika la Msaada la Sweden (SIDA) katika kipindi cha miaka mitano wametoa Sh bilioni 20 kwa ajili ya kuendeleza bunifu katika bajeti ya mwakani fedha zilizotengwa ni bilioni tisa.

Awali Mkurugenzi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dk Amosi Nungu alisema kuwa bunifu ziko katika makundi mbalimbali na wanalenga kujenga uelewa wa pamoja kwa wabunifu hao.

Mmoja wa wabunifu, Sandra Somi kutoka Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam (DIT) alisema amebuni mashine ya kumsaidia mtoto aliyezaliwa kabla ya muda kwenye upumuaji.

Alisema kuwa mashine hizo zitakuwa na uwezo wa kuokoa maisha ya watoto wengi iwapo ubunifu huo utaingia sokoni.

"Mashine kama hizo huagizwa nje ya nchi lakini zikitengenezwa hapa hapa nchini zitaokoa maisha ya watoto wengi, tunatarajia kupata teknolojia zaidi ya kuiboresha ili iingie sokoni," alisema.

Ally Mohamed kutoka Pemba alisema amebuni kifaa cha umwagiliaji na ufugaji katika bwawa la samaki.

"Tanzania ina vyanzo vingi vya maji, mabwawa kifaa nilichobuni kitasaidia sana wakulima kwenye umwagiliaji na itazisaidia hata Manispaa kwenye mifumo ya maji taka," alisema.

Dk Saidi Ally ambaye ni Mkurugenzi wa Mitihani kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) alisema kuwa amebuni mfumo wa mitihani.

Alisema kupitia mfumo huo mwanafunzi atafanya mtihani akiwa mahali popote na ni mfumo rahisi kwa gharama nafuu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live